HALMASHAURI YA WILAYA YA KISHAPU
| |
| |
TANGAZO LA KAZI ZA MKATABA
Mkurugenzi mtendaji Wilaya ya Kishapu anawatangazia wananchi Raia wa Tanzania wenye sifa ya kuomba nafasi za kazi za mkataba kama ifuatavyo:-
- Msaidizi wa Hesabu ( Accounts Assistant ) – Nafasi 4
- Sifa za Mwombaji
- Elimu ya Kidato cha nne
- Wenye cheti cha ATEC level II au “Foundation Level” kinachotolewa na NBAA.
- Majukumu/Kazi atakazokuwa anafanya
- Kuandika na kutunza “Register” zinazohusu shughuli za uhasibu.
- Kuandika hati za malipo na hati za mapokezi ya fedha.
- Kutunza majalada ya Kumbukumbu ya hesabu.
- Kupeleka nyaraka/barua za Uhasibu Bank.
- kufanya usuluhisho wa masurufu, karadha, hesabu za banki na Amana.
- Ngazi ya Mshahara
- mwombaji atayaebahatika kuajiriwa kwa mkataba ataanza na Mkataba wa malipo ya Tshs. 390,000 kwa mwezi ngazi ya TGS B
- Masharti ya jumla ya muombaji kazi ya Mkataba.
- Awe Raia wa Tanzania.
- Awe na miaka 18-45.
- Awe hajawahi kufukuzwa kazi, kupunguzwa, kuachishwa au kustaafishwa kazi katika Utumishi wa Umma.
- Awe tayari kufanya kazi kituo chochote cha Afya ndani ya Wilaya ya Kishapu.
- Mkataba utakuwa ni wa mwaka mmoja mmoja kwa kipindi chote cha mfadhili na Mkataba utarudiwa kulingana na utendaji kazi na maadili ya mtumishi.
- Kipindi cha mfadhili kikikoma mtumishi hataingizwa moja kwa moja kwenye Ajira za Serikali.
- Waombaji waambatishe vivuli vya vyeti vya Shule, Taaluma, Kuzaliwa na vitambulisho vya Taifa kwa wale walioandikishwa.
- Kila mwombaji aambatishe na picha ndogo 2 passport size zilizopigwa hivi karibuni.
- Siku ya usaili kila mwombaji afike na vyeti halisi vya shule, Taaluma, kuzaliwa na kitambulisho.
- Kila mwombaji aandike kwa ushihi anwani yake na namba ya simu inayopatikana muda wote kwa ajili ya mawasiliano.
- Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 27/07/2017
- Maombi yote yaandikwe kwa mkono bila kuchapwa.
- Maombi yote yawasilishwe kwa anwani ifuatayo:-
Mkurugenzi Mtendaji (W)
S.L.P 1288
KISHAPU
NB: Masharti yaliyoainishwa kwenye Tangazo hili yasomwe kwa makini na yazingatiwe- Stephen M. Magoiga
- Mkurugenzi Mtendaji (W)
- KISHAPU
- Nakala:
- Katibu Tawala (M) – Kwa taarifa
- Mkuu wa Wilaya
- Waheshimiwa Madiwani – Watangazieni wananchi
- Watendaji Kata Wote – Tangazeni mbao za Matangazo
- Mbao za Matangazo zote Halmashauri ya Wilaya Kishapu.
0 Comments