Subscribe Us

header ads

NAFASI ZA KAZI WILAYA YA ROMBO, TUMA MAOMBI KABLA YA TAREHE 17 SEPTEMBER 2017

Image result for JOBS

NAFASI ZA KAZI WILAYA YA ROMBO

Mkurugenzi metendaji wa Hlmashauri ya Wilaya ya Rombo anakaribisha maombi ya Watanzania  wenye sifa kujaza nafasi zifuatazo

1. DEREVA DARAJA LA II (DRIVER GRADE II). NAFASI 1

Sifa za kuingilia moja kwa moja.
i.    j.    Kuajiriwa wenye cheti cha mtihani wa kidato cha nne (IV), Wenye leseni daraja la C, C1, C2, na C3 ya uendeshaji pamoja na uzoefu wa kuendesha magari kwa muda usiopungua miaka mitatu bila kusababisha ajali, Wenye cheti cha majaribio ya ufundi daraja la II au "Level II"
ii.    Umri 21- 44
iii.    Kazi(Majukumu ya kufanya:
a) Kuendesha magari ya abiria na malori
b)    kuhakikisha gari na vyombo vyake vipo katika hali nzuri wakati wote, na kufanya uchunguzi wa gari kabla na baada ya safari ili kugundua ubovu unaohitaji matengenezo .
c)    kufanya matengenezo madogo madogo katika gari
d)    kutunza na kuandika daftari,la safari "Log- Book" kwa safari zote

MSHAHARA: Ngazi ya Mshahara wa Serikali TGOS. A

2. KATIBU MAHSUSI DARAJA LA III NAFASI MOJA (1)

SIFA ZA MUOMBAJI;
Wenye elimu ya kidato cha nne (IV), waliomaliza mafunzo ya uhazili na kufaulu mtihani wa Hatua ya Tatu. Wawe wamefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 80kwa dakika moja na wawe wamepata mafunzo ya Kompyuta kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali na kupata cheti katika Programu za Windows, Microsoft Office, Internet, E-mail na Publisher.

KAZII MAJUKUMU YA KUFANVA
i.    Kuchapa barua, taarifa na nyarakaza kawaida
ii.    Kusaidia kupokea wageni na kuwasaili shida zao, na kuwaelekeza sehemu wanayoweza kushughulikiwa.
iii.    Kusaidia kutunza kumbukumbu za matukio, miadi, wageni, tarehe za vikao, safari za Mkuu wake na ratiba ya kazi zingine zilizopangwa kutekelezwa katika ofisi anamofanyia kazi, na kumuarifu Mkuu wake kwa wakati unaohitaji   
iv.    Kusaidia kutafuta na kumpatia mkuu wake majalada, nyaraka au kitu chochote kinachohitajika katika shughuli za kazi hapo ofisini.
v. Kusaidia kufikisha maelekezo ya Mkuu wake w akazi kwa wasidizi wake na pia kumuarifu kuhusu taarifa zozote anazokuwa amepewa na wasaidizi hao.
vi.    Kusaidia kupokea majalada, kuyagawa kwa Maofisa waliokatika sehemu alipo, na kuyakusanya, kuyatunza na kuyarudisha sehemu zinazohusika.
vii.    Kutekeleza kazi zozote atakazokuwa amepangiwa na Msimamizi wake wa kazi

MSHAHARA
Ngazi Ya Mshahara Wa Serikali Yaani TGS B.

3. MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III. (VILLAGE EXECUTIVE III) NAFASI 22.

Sifa za kuingilia moja kwa moja:
1 Kuajiriwa wenye elimu ya kidato cha nne (IV)au sita (VI) aliyehitimu mafunzo ya Astashahada/ Cheti katika moja ya fani zifuatazo:
Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya Sanaa kutoka Chuo cha Serikaliza Mitaa Hombolo, Dodoma au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.

Kazi/Majukumu ya kufanya:
a)    Afisa Masuhuli na Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Kijiji .
b)    Kusimamia ulinzi na usalama wa raia na mali zao, Kuwa Mlinzi wa Amani na Msimamizi wa Utawala Bora katika kijiji
c)    Kuratibu na kusimamia upangaji wa utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo ya Kijiji.
d)    Katibu wa Mikutano na Kamatl zote za Halmashauri ya Kijiji
e)    Kutafsiri"na kusimamia Sera. Sheria na Taratibu
f)    Kuandaa Taarifa za Utekelezaji wa kazi katika eneo lake na kuhamasisha wananchi katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, umaskini na kuongeza uzalishaji mali
g)    Kiongozi wa wakuu wa Vitengo vya Kitaalam katika Kijiji.
h)    Kusimamia. kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na nyaraka za Kijiji.
i)    Mwenyekiti wa Kikao cha Wataalamu waliopo katika Kijiji
j)    Kupokea, kusikiliza na kutatua'jualalamiko na migogoro ya Wananchi
k)    kusimarnia utungaji wa sheria ndogoza kijiji.
l)    Atawajibika kwa Mtendaji wa Kata.

MSHAHARA: Ngazi ya Mshahara wa Serikali TGS.B

MASHARTI YA JUMLA
- maombi yatumwe yakiwa yameambatanishwa nakala  (certified copy) za vyeti vya elimu ya mafunzo na maelezo binafsi pamoja na passport size 1 cheti cha kuzaliwa  na majina ya wadhamini  wawili anuani zao na namba zao za simu
- waombaji ambao ni watumishi wa Umma barua zao zipite kwa waajiri wao
- waombaji wawe raia wa Taznania
- nafasi itakayoombwa ianishwe juu ya bahasha
- muombaji awe na umri wa miaka 18 - 45

Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe  17/09/2017

maombi yatumwe kwa
MKURUGENZI MTENDAJI,
HALMASHAURI YA WILAYA YA ROMBO,
S.L.P 52,
MKUU - ROMBO

Post a Comment

0 Comments