Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Waajiri mbalimbali Serikalini anapenda kuwataarifu waombaji kazi wote walioomba kazi ya Udereva zilizotangazwa tarehe 25 Julai, 2017 likiwa na kumb. Na.EA.7/96/01/I/68kuwa Usaili kwa Vitendo (Practical Interview) unatarajiwa kufanyika 15 – 19 Septemba, 2017 katika Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) kilichopo chang’ombe jijini Dar es Salaam. Wasailiwa wataofaulu usaili huo watafanya Usaili wa ana kwa ana (Oral Interview) kuanzia tarehe 28 Septemba, 2017 katika Ofisi za Sekretarieti ya Ajira zilizopo katika Jengo la Maktaba Kuu ya Taifa.
0 Comments